Zitto Kabwe Ajitokeza Adai Polisi Wanamsaka..Asema Magufuli Alienda Rwanda Kujifunza Kubana Upinzania
Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto
Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za
Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu
unaotakiwa.
Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto
kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku
viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini
njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.
"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila
hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari
kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa
nini wanivizie," amesema Zitto Kabwe na kuongeza;
''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili
niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana
habari
''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa
''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa
eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa
utawala wa kidemokrasia
''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na
vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na
Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie
''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua
kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza
Kidikteta
''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG.
Kwa hali Hii anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa term moja kwa
sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa
.
''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti
''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa
wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete
mpaka nchi irudi kwenye misingi''
''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila
kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi
hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza
kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao
''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya
siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu
hamjaona hata sisimizi amekanyagwa
''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni