Diamond Platnumz hakwenda mikono mitupu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar…
Ni June 6, 2016 ambapo staa Diamond Platnumz aliungana na uongozi wake wa label ya WCB kuelekea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na waandishi wa habari RC Paul Makonda alisema….’Diamond na uongozi wake wamekuja ofisini kutoa shukrani na pia kuomba niwe kama mlezi wao wa WCB nitahusika kuwashauri na kuwaelekeza yale watakayotaka niwashauri katika kazi zao‘-Paul Makonda
‘WCB ni label ambayo ndani yake kuna vijana wanaofanya kazi zao za sanaa lakini wakiwa na malengo yakuwekeza kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha maisha yao kuongeza pia pato la uchumi wa taifa letu, sasa kwa kifupi wametoa mchango ambao unasaidia katika sekta nzima ya Elimu ambapo wametoa madawati 600 tutayapata kutoka kwao ni sehemu yao kusema asante kwa watanzania’– Paul Makonda
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni