Jumamosi, 4 Juni 2016

Habari kubwa magazetini leo;

‘Msaidizi wa Kitwanga Matatani bungeni’... Gazeti la Nipashe limeripoti kuwa siku chache baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani , Charles Kitwanga kutokana na ulevi, Naibu waziri wa Wizara hiyo, Hamad Yussuf Masauni, ameshtakiwa kwa uongozi wa bunge akidaiwa kutoa majibu ya dharau bungeni. Nipashe limesema kwamba jana June 03 2016 mbunge wa Nkasi ‘CCM’, Ally Keissy alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akidai Mhandisi Masauni amekuwa akitoa majibu ya dharau kwa wabunge. Gazeti hilo limemnukuu Keissy kuwa alidai Naibu Waziri huyo amekuwa akitoa majibu ya kejeli na kiburi na kwamba wabunge wengi hawaridhishwi na majibu yake .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni