SERIKALI HAITAMVUMILIA KIONGOZI YEYOTE ATAKAYEDONOA FEDHA ZA MICHANGO YA MADAWATI-MAJALIWA.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamchukua hatua kiongozi yeyote atakayedonoa fedha za michango ya madawati inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo.* *Pia amewaagiza watendaji wote wa Serikali, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu waWilaya na Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha michango hiyo inayotolewa inawafikia walengwa.Aidha, amezitaka wilaya zote nchini zianzishe mpango endelevu wa kuhakikisha kwamba upungufu wa madawati unasahaulika kabisa katika maeneo yao na kwamba utendaji wa viongozi wa elimu na serikali katika ngazi mbalimbali utapimwa kutokana na jinsi ambavyo wametekeleza maagizo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni