Diamond afunguka kuhusu Wema Sepetu wa sasa
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, kinachoruka kupitia EATV, Diamond alisema, “Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekua labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa.”
“Lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita,” aliongeza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni