Jumatatu, 13 Juni 2016
Zitto Kabwe Ajitokeza Adai Polisi Wanamsaka na kasema....
Adhabu 4 kwa askari wasiotoa 'saluti'
VIDEO: Adhabu 4 kwa askari wasiotoa heshima ya ‘saluti’ ikiwemo kwa wabunge
Jumamosi, 11 Juni 2016
Rita Paulsen
Video: Madame Rita kaingia rasmi kwenye utangazaji
Kassim Majaliwa na michango ya wadau
SERIKALI HAITAMVUMILIA KIONGOZI YEYOTE ATAKAYEDONOA FEDHA ZA MICHANGO YA MADAWATI-MAJALIWA.
Alhamisi, 9 Juni 2016
Hospitali ya Mwananyamala, Amana na TMK zitarajie huduma hii kutoka kwa Serikali ya Japan
Hospitali ya Mwananyamala, Amana na TMK hali kuwa safi
New justin Bieber video
Video: Justin Bieber – Company
Ever wanted to tour the world with Justin Bieber? Well, the pop heartthrob gives fans a chance to do just that in the doc-style video for “Company,” the latest single off Purpose.
VIDEO QUEEN WA NJE na HARMONIZE
HARMONISE AMESEMA GHARAMA ZINAWASABABISHA KUWATUMIA VIDEO QUEEN WA NJE.
Harmonise msanii kutoka #Wcb amesema trend iliyopo kwa sasa wasanii wengi wa bongo kutowatumia #models wa kibongo kwenye video zao inatokana na gharama za kuwasafirisha ukilinganisha na wale wanaowapata kule.
Kupitia #Planetbongo amesema game imebadilika na kila msanii anatafuta njia ya kujiweka vizuri kibiashara.
Video nyingi za wasanii wa bongo za hivi karibuni hasa zilizofanyiwa
nje ya nchi video Queen wake ni kutoka nje ya nchi na wengine ni wazungu
isipokuwa ile ya diamond ft mafikizolo ambayo mtanzania millen magese
alionekana.
Jumatano, 8 Juni 2016
Bifu ya Prezoo na jaguar
Prezzo amchana Jaguar, amuita mshamba, ni baada ya yeye kuitwa ‘socialite’ (Audio)
Tafsiri ya socialite ni: Someone who has money and doesn’t work, instead devoting his/her life to being “socially active.” Socialites go to parties, gather media attention, and essentially “work” at being popular.
“Mimi simchukii Prezzo namheshimu sana lakini akicome tufanye song aache hiyo mambo ya usocialite ana akue mwanaume,” alisema Jaguar kwenye interview hiyo.
Kwa upande wake Prezzo aliyezungumza hivi karibuni na kipindi cha Funiko Base cha Radio5, alidai kuwa hana tatizo na wazo hilo la kufanya wimbo naye lakini akamuonya apunguze kwanza ushamba.
“Akipunguza ushamba then mimi na yeye tunaweza kufanya kazi. Lakini ujue jamaa kwangu mimi ana ushamba mwingi yaani. Kuna video kafanya na Mafikizolo angalieni hiyo nyimbo. Kuna sehemu kafanya kile kitu kinachofaa kuwa dub. Ile Jaguar alivyofanya mshkaji wangu ni kama anampiga mtu kipepsi,” alisema Prezzo na kumalizia na kicheko.
Jumanne, 7 Juni 2016
Picha ya mama Maria Nyerere na Nyerere kutokezea kwenye mti
GUMZO TANGA: Picha ya mama Maria Nyerere na Nyerere kutokezea kwenye mti
Yanga imemuongezea mkataba Mbuyu Twite
Yanga imemuongezea mkataba Mbuyu Twite, lakini imemtema staa wake mmoja wa kimataifa
Masoud Kipanya akiri Maisha Plus ilipoteza mvuto baada ya kuingiza akina mama na kilimo, asema msimu mpya unarudi na burudani tena
Maisha plus sasa yarudi tena
Mchoraji maarufu wa vibonzo na mtangazaji wa Clouds FM, Masoud Kipanya amekiri kuwa misimu miwili iliyopita ya shindano la Maisha Plus ilipoteza mvuto kutokana na kuwachanganya vijana na akina mama na pia kuingiza masuala ya kilimo.
Na sasa Masoud amedai kuwa msimu mpya ambao tayari umeanza usaili utarudisha ile Maisha Plus ya awali yenye burudani zaidi.
“Msimu wa tano unarudi kwa vijana peke yao, hakuna tena kinamama, wakulima wala nani hawahusiki. Sasa hivi ni vijana peke yao. Kwahiyo ule mchakamchaka, ile burudani ya nguvu ambayo vijana walikuwa wanaipata kupitia Maisha Plus ya kwanza nay a pili sasa watakuja kuipata tena katika msimu huu wa tano,” Masoud alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Mwaka huu shindano litahusisha pia vijana kutoka Afrika Mashariki ambapo kutoka Tanzania watakuwa 14 na nchi zingine 16. Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30.
Msikilize zaidi hapo chini.
Jumatatu, 6 Juni 2016
GoodNews: A.K.A wa South Africa kapata dili la kuperform main Stage ya BET
A.K.A wa kusini mwa Africa ndani ya shavu
Tuzo za BET ni tuzo kubwa za muziki kutoka Marekani na zenye heshima kubwa duniani, ambapo mwaka huu zitafanyika June 26 2016 Los Angeles Marekani. Kama kawaida wasanii wataperform ila good news ni kutoka kwa rapper A.K.A kutoka South Africa ambaye nae anaingia katika histori ya msanii wa Afrika kupata nafasi ya kuperform kwenye main stage.
Sambamba na A.K.A wasanii wengine watakaofanya perfomance siku hiyo ni pamoja na Rapper Fat Joe, Lil Wayne ,2chainz, Fetty Wap, Desiigner na wengine wengi. A.K.A atakuwa msanii wa kwanza kutoka Africa kuperform kwenye Main stage ya tuzo za BET ikiwa inaashiria kiasi gani muziki wa Africa unazidi kufanya vizuri duniani
A.K.A atafanya show kwenye tuzo za BET June 25 2016,yaani siku moja kabla ya tuzo zenyewe kufanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater, hii ni good news nyingine kwa muziki wa Afrika baada ya siku chache Chris Brown kumualika Wizkid katika tour ya ONE HELL OF A NIGHT TOUR.
Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji wawili leo June 6 2016
Hii ndio Yanga!
Good news kwa mashabiki wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans, taarifa kutoka klabu ya Dar es Salaam Young Africans zimetolewa leo June 6 2016 kufanikiwa kuwasajili wachezaji wa wawili.
Yanga wamefanikiwa kumsajili aliyekuwa golikipwa Tanzania Prisons Beno Kakolanya na Vicent Andrew ambaye wengi wanamjua kwa jina la utani kama Dante kutoka Mtibwa Sugar kama beki wa pembeni.
Yanga kwa sasa wanajiandaa kwa ajili ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika. Hivyo usajili huo unalenga kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya kuanza kwa hatua ya Makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Yanga wataanza kucheza na Mo Bejaia ya Algeria June 17 2016.
Kauli ya Jerry Muro baada ya kupeleka vielelezo TAKUKURU kuhusu wanaohujumu Yanga
Kauli ya Jerry Muro baada ya kupeleka vielelezo TAKUKURU kuhusu wanaohujumu Yanga
“Leo tumetekeleza maelekezo ya yaliotolewa na mwenyekiti wetu, kwanza kuwasilisha tuhuma zote zilizotolewa na mwenyekiti wetu tunaziwakilisha TAKUKURU, kama unakumbuka katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya kuchukua fomu alitoa maelekezo hayo na sisi tumetekeleza”
Diamond afunguka kuhusu Wema Sepetu wa sasa
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, kinachoruka kupitia EATV, Diamond alisema, “Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekua labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa.”
“Lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita,” aliongeza
Diamond Platnumz hakwenda mikono mitupu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar…
Ni June 6, 2016 ambapo staa Diamond Platnumz aliungana na uongozi wake wa label ya WCB kuelekea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na waandishi wa habari RC Paul Makonda alisema….’Diamond na uongozi wake wamekuja ofisini kutoa shukrani na pia kuomba niwe kama mlezi wao wa WCB nitahusika kuwashauri na kuwaelekeza yale watakayotaka niwashauri katika kazi zao‘-Paul Makonda
‘WCB ni label ambayo ndani yake kuna vijana wanaofanya kazi zao za sanaa lakini wakiwa na malengo yakuwekeza kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha maisha yao kuongeza pia pato la uchumi wa taifa letu, sasa kwa kifupi wametoa mchango ambao unasaidia katika sekta nzima ya Elimu ambapo wametoa madawati 600 tutayapata kutoka kwao ni sehemu yao kusema asante kwa watanzania’– Paul Makonda
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Jumapili, 5 Juni 2016
School Is Not For Everone, Dropping Out Helped Me Find Myself – Brymo
Singer, Olawale Ashimi, has caused a major uproar on twitter following his response to a fan who asked for his help.
Earlier today, a fan had asked Brymo for assistance in paying in his fees and the ‘Happy Memories’ crooner, replied that its ebst for the fan to drop out as education isn’t for everyone.
The former Chocloate City act, further added that he dropped out of school as well, which ended up having positive impact in his life as he is today one of the finest musicians in the country.
With some fans agreeing with his ideology, others took time to blast him severely.
Hakuna tena bado nipo nipo: Mwana FA afunga ndo
Mwana FA unaona lini? Hatimaye jibu lake limepatikana. Rapper huyo amefunga ndoa Jumapili hii.
Hitmaker huyo wa Asanteni kwa Kuja amefunga ndoa na mchumba wake aitwaye Helga.
Ndoa hiyo ya kiislamu imehudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu wakiwemo AY, Hermy B, Ommy Dimpoz, Sallam, Dully Sykes, Alberto Msando na wengine.
Tunampongeza FA kwa hatua hiyo.
Majibu ya Sober House’ Baada ya Taarifa za Chid Benz kutoroka kituoni hapo kusambaa
March 22, 2016 meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale alimpeleka msanii wa muziki wa Hip Hop
kutoka Ilala, Rashid Makwilo aka Chid Benz Sober House iliyopo Bagamoyo iitwayo
Life and Hope Rehabilitation Centre kwaajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia
madawa kulevywa na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.
Headline za kutoroka kwa msanii huyo kwenye nyumba hiyo ya kuhudumia
waathirika wa dawa za kulevya zilianza baada ya watu kumuona msanii huyo
akiwa mtaani June 5 2016 Mkuu wa Kituu hicho cha Sober House ameelezea ukweli
wa msanii Chid Benz kwenye kituo hicho.
Mkuu wakituo hicho cha kusaidia watu walioathirika na matumi ya dawa za kulevywa Al-Kareem Bhanji amekanusha
taarifa hizo na kusema kuwa Chid Benz ameruhusiwaa kutoka baada ya afya yake kuimalika.
ukweli ni kwamba chid benzi hakutoloka kituoni alitoka kwa kufuata taratibu zote na baraka za uongozi baada ya
kuoekana yupo sawa kwa mant’iki hiyo naomba vyombo vya habari mpuuze taarifa za kuwa alitoroka kituoni’>>>Al-Kareem Bhanji .
Kuhusu Babu tale kumtelekeza Chid Benz kituoni taarifa hizo siza kweli kwani babutale ndio aliyemfuata chid
kituoni siku ameruhusiwa na alikuwa anatoa ushurikiano wakati wowote pale atakama ni usiku manane.
Rais Magufuli ashiriki ibada katika kanisa la "Mzee wa Upako"
Jumapili hii Rais Magufuli amehudhuria ibada katika Kanisa la Mchungaji Lusekelo maarufu kama "Transfoma" au "Mzee wa Upako" eneo la Ubungo-Kibangu Hii ni kama "desturi" aliyoanza kujiwekea kwa kusali katika makanisa ambayo siyo dhehebu lake,mara ya mwisho Rais alijumuika na waumini wa kanisa la KKKT usharika wa Azania Front
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam na kuwaahidi waumini wa kanisa hilo kuwa Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambako itaungana na barabara ya Mandela. Rais Magufuli ambaye amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo iliyofanyika leo tarehe 05 Juni, 2016 amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine wa eneo la Ubungo Kibangu kwa lengo la kujionea hali halisi. Aidha, Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako kwa huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake vya Mahubiri kupitia Luninga. “Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo nataka kukuthibitishia ninakupenda sana. “Ndio maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo” Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini. Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha viwanda.
Rich Mavoko – Ibaki Story | Lyrics/Mashairi
[Verse 1]
Matapishi ni kinyaa kuzirudisha tena kwenye kinywa Japo mengi ulisema, kama nuru ghafla ukazima Ikawa ngumu kukusahau, nikasema moyo ukome Kwa kali sulu na madharau, penzi ulivunja na ngome
[Pre-Chorus]
Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto
[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe
[Verse 2]
Kiliniumiza kitanda na shuka tuliolalia Mapenzi yana siri kubwa, sishangai mtu akilia Nimekubali mboni zangu zimtazame mwingine Maridhia ya moyo wangu huenda si fungu pengine Cha kushangaza hadharani mengi ya kuficha ukaweka wazi Nikahisi sijui mapenzi, labda kwako sinogi nazi
[Pre-Chorus]
Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo Aa ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo Leo unatamani wewe kurudia zamani, ni ndoto Wewe nirubuni kwa penzi la kidani kama mtoto
[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe
[Bridge]
Yalinitesa mazoea aya Lakini mi nishazoea mwaya Ila tambua mapenzi mabaya Kidonda chake hakinaga dawa Ee mazoea aah Lakini mi nishazoea mwaya Ila tambua mapenzi mabaya Kidonda chake hakinaga dawa
[Chorus]
Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, uuh uuh Mi na wewe, acha ibaki story mi na we Mapenzi mi na wewe, uuh uuh
HII NDIO ZAWADI YA BIRTHDAY YA NAY WA MITEGO MWAKA HUU…!!
Katika kusherehekea birthday yake mwaka jana, msanii Nay Wa Mitego alihamia katika nyumba yake mpya ya Kimara huku akijizawadia gari mpyaaaa. Habari hiyo ilikua gumzo sana magazetini na mitandaoni kwani nyumba hiyo ilikua ya kisasa kabisa. Tarehe 9 mwezi huu Nay Wa Mitego atasherehekea siku yake ya kuzaliwa na moja kati ya maswali yaliyokua yakimuumiza
Rais wa Angola amteua binti yake ambaye ni mwanamke tajiri Afrika kuwa mkuu wa shirika la mafuta la serikali
Rais Jose Eduardo dos Santos amemteua binti yake, Isabel kuwa mkuu wa shirika la mafuta linalomilikiwa na serikali, Sonangol.
Angola, kumiliki visima vya mafuta ni sawa na kuitawala nchi. Uteuzi huo wa binti yake ni dalili za kutaka kutafuta maboresho kwenye sekta hiyo ya mafuta inayododa nchini humo. Lakini wakosoaji wanadai hakuna lolote bali ni janja ya rais huyo anayetuhumiwa kwa ufisadi mkubwa kuvuna utajiri zaidi. Dos Santos ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 36, ni rais wa pili Afrika aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi. Ameahidi kuachia madaraka mwaka 2018.
Isabel dos Santos, 43, ana utajiri wa dola bilioni 3.3 ambao unahusishwa na mali za serikali. Mali zake ni pamoja na kumiliki asilimia 25 ya shirika la mawasiliano ya simu Angola, Unitel. Pia anamiliki asilimia 7 ya shirika la mafuta la Ureno, Galp Energia, hisa kwenye kampuni ya runinga ya Ureno pamoja na hisa nyingi kwenye moja ya benki kubwa za Angola, Banco BIC na mwingine. Hisa zake 18.6% kwenye benki ya pili kwa ukubwa Ureno, BPI zinauzwa. Isabel dos Santos pia anamiliki maduka kibao na klabu ya usiku. Sonangol inasimamia hazina kubwa ya mafuta na gesi nchini Angola na inachangia nusu ya pato la taifa.
Wakati huo huo kaka zake, Welwitchea José dos Santos na José Paulino dos Santos wanamiliki Semba, kampuni ya mawasiliano ambayo hupewa tenda za serikali katika miradi ya masoko na matangazo. Semba imekuwa ikituhumiwa kwa kupokea fedha moja kwa moja kutoka kwenye bajeti ya serikali.
Rich Mavoko: Mkataba wangu na King Kaka haukuwa na limitation
Msanii mpya wa lebo ya Wasafi, Rich Mavoko amefafanua mkataba wake wa mwanzo aliosaini na menejimenti ya King Kaka
Rich Mavoko kwa sasa amefanikiwa kusaini mkataba mpya wa miaka 10 na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond. Akiongea kwenye kipindi cha XXL, kinachoruka kupitia Clouds FM, Rich Mavoko alisema kuwa makubaliano yake na King Kaka hayakuwa na limitation yeyote.
“Nafikiria yalikuwa ni makubaliano tu hayakuwa na limitation yeyote, muda wowote kama mimi sijaridhika ninaweza nikatengua makubaliano hayo. Kwahiyo tukapatana nikatengua makubaliano hayo before hata kuingia wasafi,” aliongeza.
Jumamosi, 4 Juni 2016
Tanzania imetolewa na Misri michuano ya AFCON 2017 leo June 4
June 4 2016 ilikuwa ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wake wa tatu wa Kundi G wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 AFCON, kwa kucheza na timu ya taifa ya Misri The Pharaos uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Huu ni mchezo ambao Taifa Stars alikuwa anahitaji ushindi wa aina yoyote ile
Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu kwa Taifa Stars, lakini ulikuwa ni mchezo wa marudiano na timu ya taifa ya Misri baada ya mchezo wa kwanza kuchezwa Misri June 14 2015 katika mji wa Alexandria na kumalizika kwa Taifa Stars kufungwa jumla ya magoli 3-0, hivyo huu ulikuwa ni mchezo wa kulipa kisasi kwa Taifa Stars, lakini pia ulikuwa ni mchezo wa kutengeneza mazingira ya kufuzu AFCON 2017.
Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania licha ya kuwa nyumbani imekubali kipigo cha goli 2-0, , magoli ya Misri yalifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea anayeichezea klabu ya AS Roma ya Italia Mohamed Salah dakika ya 43 na 58, kwa upande wa Tanzania Mbwana Samatta alikosa penati iliyopatikana baada ya Himid Mao kufanyiwa faulo ndani ya 18.
Kwa matokeo hayo Taifa Stars wanakuwa wametolewa rasmi katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017, lakini imebakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba itakayocheza September dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Misri imefikisha jumla ya point 10, Taifa Stars point moja na Nigeria ina point 2.
Irene Uwoya kuja na tamthilia yake mpya iitwayo ‘Drama Queen’
Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Uwoya amesema tamthilia kwa sasa zinalipa vizuri kutokana na runinga nyingi kuhitaji tamthilia. “Nataka kufanya tamthilia ambayo inaitwa Drama Queen,” alisema Uwoya “Mimi ndio Drama Queen mwenyewe, na niliamua tu kufanya kitu tofauti ili kuleta ushindani katika game.”
Katika hatua nyingine, Irene Uwoya amewataka mashabiki wake kusubiria kazi zake mpya za filamu ambazo atazitangaza hivi karibuni.
Linah asema amefurahi kuona Ex wake anafunga ndoa na mwanamke mwingine
Msanii wa muziki, Linah Sanga amesema anampongeza Ex wake kwa kufunga ndoa na mwanamke mwingine kwani anaamini hiyo haikuwa bahati yake.
LINAH NANAGARIAkiongeza na Bongo5 Alhamisi hii, Linah amesema licha ya kuachana na Ex wake huyo miezi kadhaa iliyopita, lakini bado alikuwa anawasiliana naye na taarifa za kufunga ndoa alikuwa yazo.
“Katika hali ya kawaida nimejisikia poa kwa sababu nilishaacha naye, kwa hiyo mimi nilikuwa namtakia mazuri siku zote, na ndo maana tulikuwa washikaji,” alisema Linah.
Pia Linah amesema wakati Ex wake anafanya mipango ya kuoa alikuwa anawasilianaye pamoja na kupewa taarifa mbalimbali ya vitu vinavyoendelea.
Pia muimbaji huyo wa wimbo ‘Ole Themba’, amesema alishindwa kuhudhuria ndoa ya Ex wake kutokana na kuwa busy na kazi.